Akihutubia wanafunzi hao, Sheikh alisisitiza kuwa: “Mwanamke ni nusu ya jamii. Ikiwa mwanamke ataelimika vyema na kuadabika kwa adabu na akhlaq njema za kidini, basi jamii nzima itakuwa imeelimika kwa asilimia mia moja.”

9 Novemba 2025 - 16:10

Sheikh Swahibu Shabani atembelea Hawza ya Mabinti wa Kiislamu – Arusha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Samahat Sheikh Swahibu Shabani, ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa wa Tabora kupitia Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C) na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Taifa, amefanya ziara maalumu katika Hawza ya Mabinti wa Kiislamu iliyo chini ya Taasisi ya Sayyid al-Shohadaa (a.s.), jijini Arusha.

Sheikh Swahibu Shabani atembelea Hawza ya Mabinti wa Kiislamu – Arusha

Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhamasisha maendeleo ya kielimu na kiroho kwa mabinti wa Kiislamu, Sheikh Swahibu alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa Hawza hiyo na kuwapa nasaha muhimu kuhusu elimu ya dini, maadili mema, na mustakbali wao wa baadaye.

Akihutubia wanafunzi hao, Sheikh alisisitiza kuwa: “Mwanamke ni nusu ya jamii. Ikiwa mwanamke ataelimika vyema na kuadabika kwa adabu na akhlaq njema za kidini, basi jamii nzima itakuwa imeelimika kwa asilimia mia moja.”

Aliongeza kuwa, jukumu la mwanamke katika jamii ya Kiislamu ni kubwa na lenye thamani, hivyo ni wajibu kwa mabinti wa Kiislamu kujituma katika elimu, kushikamana na misingi ya dini, na kuwa mfano bora wa mwenendo mwema katika familia na jamii kwa ujumla.

Sheikh Swahibu pia aliipongeza Taasisi ya Sayyid al-Shohadaa (a.s.) kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuwalea na kuwaendeleza kielimu na kiroho mabinti wa Kiislamu, akibainisha kuwa taasisi kama hizi ni nguzo muhimu katika kuendeleza elimu ya dini nchini Tanzania.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa dua na mazungumzo ya kirafiki kati ya uongozi wa Taasisi, walimu, na wanafunzi, ambapo wote walieleza furaha na shukrani zao kwa ziara hiyo yenye baraka na hamasa.

Sheikh Swahibu Shabani atembelea Hawza ya Mabinti wa Kiislamu – Arusha

Your Comment

You are replying to: .
captcha